Our Teachers

DSC01571

HEAD TEACHER / MWALIMU MKUU

Pontian Celestine Kanyoro, age 32, teacher.

During my life I want to accomplish the following things:
After one year:
– Marry and have two children two and a half years apart.
After five years:
– Build a good home.
– Plant trees to protect the environment and to earn some extra income. I especially want to plant fruit trees for good health.
– To raise livestock like goats and cows for food and extra income.
– To visit my friends in various countries like the US, China, England, Kenya, Uganda, South Africa and Japan so that we can trade ideas and learn more from each other.
After 10 years:
– To work together with friends and other education stakeholders to start a school for elementary school students with the goal of helping them discover, increase and develop their talents.

I value humanity as a whole and each individual person, equality, justice, friendship and love.

My talents are creativity; to instruct, teach and motivate my community; to play and teach sports such as soccer, netball, volleyball, track and field, swimming, etc.

At the end of my life, I hope to have accomplished many things, such as:
– To have started a school to help students discover and develop their talents in order to help themselves, their families and their community.
– To have helped achieve the dream of spreading justice and equality across the world so that every being is happy and living in peace.
– To have created many new things that will help bring respect and value to the lives of all creatures.

Pontian Celestine Kanyoro, miaka 32, mwalimu.

Katika maisha yangu nataka kufanya yafuatayo:
Baada ya mwaka mmoja:
– Kuoa mke mzuri mwenye nidhamu na kuzaa watoto wawili watakaopishana kwa miaka miwili na nusu.
Baada ya miaka mitano:
– Kujenga nyumba bora ya kuishi.
– Kupanda miti kwa lengo la kuhifadhi mazingira na kwa ajili ya kipato. Pia miti ya matunda kwa ajili ya afya bora.
– Kufuga mifugo kama ng’ombe na mbuzi kwa ajili ya chakula na kukuza uchumi.
– Kutembelea marafiki wan chi mbalimbali kama USA, China, Uingereza, Kenya, Uganda, Afrika Kusini na Japani kwa ajili ya kubadilishana uzoefy na kujifunza zaidi.
Baada ya miaka kumi:
– Kuanzisha shule ya watoto wadogo kwa lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto wadogo. Hii ni kwa kushirikiana na marafiki na wadau mbalimbali.

Mie nathamini utu wa mtu, usawa, haki, urafiki na upendo.

Vipaji nilivyo navyo ni pamoja na : Ubunifu ; kufundisha, kuelimisha na kuhamasisha jamii ; kucheza na kufundisha michezo kama football, netball, volleyball, track and field events, swimming, n.k.

Mwisho wa maisha yangu natumaini niwe nimetimiza mambo kadha kama :
– Niwe nimeanzisha shule ya kuibua na kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto wadogo kwa faidha yao wenyewe, familia yao na jamii kwa ujumla.
– Niwe nimetimiza ndoto ya kuleta haki na usawa duniani ili kila kiumbe hai kifurahie haki ya kuishi kwa amani.
– Niwe nimebuni vitu vipya vyingi ambavyo vitasaidia kuyapa heshima na thamani maisha ya viumbe hai.

 

GROUP LEADERS / VIONGOZI WA MAKUNDI

Fahim Ally

DSC01636First and foremost, I am a young Tanzanian who loves his country and fellow citizens. There are many things I value in life, and I have various goals that I often think about and am determined to achieve during my lifetime. These things, which I would like to officially pronounce, are as follow:

Things I love in my life: First I love to study and to understand, to build friendships with different people from different countries, to help my family and my community as a whole, to exercise and to dance. For sports, I love volleyball and wrestling. Concerning food, I love to eat bananas, ugali, rice, spinach and spaghetti and to drink a lot of water. Concerning my studies, I love studying art and sciences like chemistry, geography and biology.

Things that I value in my life: Foremost I value the lives of all people. I value using time productively, food, water and human rights. I value children, my parents, my relatives, my friends and my community as a whole. Finally, I value farming, education and the environment.

I believe in various things, such as: Water is life for plants and animals. All people are entitled to the same basic rights. I also believe all people can accomplish anything they want if they have a plan and stick to it. I also believe agriculture is the backbone of our country because every day we depend on agriculture for life. Finally, I believe in Almighty God because he alone is all powerful.

Concerning my skills: I have many skills, including running, singing, dancing, playing volleyball and acting. I am also good at making friends because of the love I show for all people.

Concerning my life goals: First and foremost I have the goal of being a person who helps his community deal with the universal issue of education and who is an excellent worker for all my jobs, whether they be temporary or long term. Concerning my studies, I hope to go to university and study what I choose, perhaps animal husbandry and agriculture.

Concerning my responsibilities: For now my responsibilities include being a good-hearted, loyal, upright person who respects others and the values of my country. I also have the responsibility to help my parents, relatives, friends and other people with whatever they may need. I also have the responsibility of ensuring that I will achieve my goals and dreams in various areas, such as in my studies.

Finally, I hope that I will have accomplished all of the goals that I have mentioned above before leaving this life. Last of all, I would like to mention the most important person in my life: my mother, who I love very much.

Kwanza kabisa, mimi ni kijana wa kitanzania anayependa nchi yangu na raia wenzangu. Ndani ya maisha yangu nina vitu mbalimbali ninavyovifikiria na kuazimia kuvitimiza kipindi cha uhai wangu. Vitu hivyo nivitamke rasmi kama ifuatavyo :

Mambo ninayopenda maishani mwangu : Kwanza kabisa ninanpenda kusoma na kuelewa, kujenga urafiki na watu mbalimbali kutoka nchi tofauti, kutoa msaada kwa familia yangu na jamii kwa ujumla, kufanya mazoezi ya viungo vya mwili, michezo na muziki. Kwa upande wa michezo ninapenda sana mchezo wa mpira wa wavu, kukimbia na mieleka. Na upande wa chakula ninapenda kula ndizi, ugali, wali, mboga za majani, tambi sambamba na maji mengi ya kunywa. Pia upande wa masomo ninayapenda sana masomo ya sayansi na sanaa kama chemia, jiografia na baiolojia ya wanyama na mimea.

Mambo ninayothamini maishani mwangu : Kwanza kabisa ninathamini uhai wa mtu yeyote. Ninathamini matumizi ya muda, chakula na maji, haki za binadamu sabamba na elimu kwa ujumla. Na mwisho ninawathamini watoto, wazazi wangu, ndugu, marafiki na wanajamii kwa ujumla. Mwisho kabisa ninathamini sana kilimo, elimu na mazingira kwa ujumla.

Ninamini katika mambo na vitu mbalimbali kama vile : Maji ni uhai wa wanyama na mimea, haki za binadamu ni sawa kwa kila mtu, pia ninamini kwa kila mtu akipanga kitu au mpango anaweza kufanya na kufanikiwa. Na pia ninaamini kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu kwani kila sika tunategemea kilimo ili tuweze kuishi vizuri. Na mwisho ninaamini juu ya mwenyezi mungu kwani yeye ndiye mweza wa yote.

Na kwa upande wa vipaji : Nina vipaji mbalimbali kama vile kukimbia, kuimba na kucheza muziki, kuchezo mpira wa wavu, kuigiza na pia nina kipaji cha kupendwa na watu mbalimbali kulingana na upendo ninaowaonyesha.

Kwa upande wa malengo yangu ya maisha : Kwanza kabisa nina lengo kuu la kuwa mtu mwenye msaada mkubwa kwenye jamii kwenye swala zima la utoaji wa elimu mbalimbali, kuwa mfanyakazi bora pindi nitakapopata kazi iwe ya muda mfupi au mrefu. Kwa upande wa masomo natumaini kusoma mpaka chuo kikuu kwa kitu ninachokuwa nasomea, mfano wanyama na mimea ikiwemo ufugaji na kilimo.

Pia kuhusu majukumu yangu : Kwas sasa majukumu niliyonayo ni kama vile kuwa mwema, mtiifu, mwadilifu, mwenye heshima na busara, kuheshima tunu za taifa ndani ya jamii. Na pia nina jukumu la kutoa msaada wowote unapohitajia kwa wazazi, ndugu, rafiki na watu wengine kama inawezekana. Pia nina jukumu la kuhakikisha ninatimiza malengo yangu na matakwa yangu katika nyanja mbalimbali kama vile masomo yangu.

Mwisho kabisha ninatumaini nitakuwa nimetimiza hayo yote niliyoyatamka kabla ya kupoteza uhai wangu. Na mwisho kabisa natamka rasmi mtu muhimu maishani mwangu : mama yangu nampenda sana.

Happiness Henry

DSC01629My name is Happiness Henry, and I live in the Bomani area of Kayanga, Karagwe, Tanzania.

Right now I am an 11th grade student at Kabango Secondary School in the Ngara disctrict in the Kagera region. Currently I am focused on my education. I strive to study hard so that in the future I will be able to live a good life and help those in need.

The things I value in life are human dignity, my one parent who remains – my mother and all other people, whether they be young or old, poor or rich. I also value equality and rights for all people, my health and the health of others. I also value any job I might have for any length of time.

I hope that after my studies I will be an excellent, dedicated, dependable worker who has good manners and is able to work well with others. If we can all achieve these things our community will develop.

I have the following skills: I am good at teaching about biology and the environment; I love to create many things using paper, tree leaves and banana leaves; I exercise and am in good shape.

For now I am a student so my main responsibility is to study. However, during this school break I have had the good luck to be employed by The Ota Initiative in Kayanga, Karagwe. This organization is here to help small children. Ota aims to help children: to think critically, which will help them do well in school and in life in general; to be creative and to value their own ideas; and to be confident and share their ideas with others. It also motivates children to love arts and science.

My short term goal is to study hard so that I will be able to go to college in 2015. My long-term goal is to be a health worker and to help change the condition of life here, which is to say to help improve the low quality of life so people have better lives.

At the end of my like I would like to have done the following things: to have obtained a good home to live in; to have provided for all of my mother’s needs so that she can relaz because she has worked hard from the day I was born and even now she continues to help me; to have obtained a car or other mode of transportation; to have helped those in need like orphans, widows, people with disabilities and the elderly; to have helped all other people who might have been in need of my assistance.

Finally, I would like have a small family that will live together in love, peace, unity and communion with the love of our God.

Mimi ninaitwa Happiness Henry. Ni raia wa Tanzania. Naishi katika Hlmashauri ya wilaya ya Karagwe, Kata ya Kayanga, mtaa wa Bomani.

Hivi sasa ni mwanafunzi wa darasa la kumi na nne katika Shule ya Sekondari ya Kabanga iliyopo wilayani Ngara katika mkoa wa Kagera. Ninatafuta elimu katika maisha yangu ya sasa. Ninajitahidi kusoma kwa bidii ili hapo mbeleni niweze kuishi maisha bora pia kuwasaidia wahitaji.

Mambo ninayoyathamini ni pamoja na utu wangu, mzazi wangu niliyebaki naye kwas asa ambaye ni mama yangu, ninawathamini watu wote, wakubwa kwa wadogo, maskini kwa matajiri. Ninathamini sana usawa na haki za binadamu, afya yangu na afya za wengine. Pia nathamini kazi niliyonayo kwa wakati muafaka.

Ninaamini kuwa baada ya masomo yangu nitaweza kuwa mfanyakazi bora, mtiifu, mwenye nidhamu, pia kushirikiana na wenzangu vizuri, kuwa mwaminifu, na hayo yote yakifanikiwa naamini tutapata jamii yenye maendeleo.

Vipaji nilivyonavyo ni kama ifuatavyo : Ninaweza kufundisha vizuri somo la elimu ya viumbe hai, mazingira na pia napenda sana kubuni maumbo mbalimbali kwa kutumia vitu kama karatasi na majani ya miti na migomba. Pia ni mwanamazoezi ya mwili.

Kwa sasa mimi ni mwanafunzi, hivyo jukumu langu kibwa ni kusoma. Lakini pia katika kipindi hiki cha likizo ndefu, nimepata bahati nzuri ya kufanya kazi na shirika la The Ota Initiative lililopo Kayanga, Karagwe. Shirika hili lipo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wadogo. Shirika hilo la Ota linalenga kumfanya mtoto awe na uwezo wa kufikiri kwa kina ambao utamsaidia kufanya vizuri katika taaluma yake na maishani mwake kwa ujumla , kumfanya mtoto awe mbunifu na kuthamini mawazo yake pia kumpatia ujasiri wa kutoa mawazo yake. Pia kumhamasisha mtoto kuipenda sayansi na sanaa.

Malengo yangu ya muda mfupiani kusoma kwa bidii ili niweze kujiunga na chuo kikuu 2015. Na malengo yangu ya muda mrefu ni kuwa mhudumu katika sekta ya afya na kufanya mabadiliko katika hali ya maisha yaani kutoka katika hali duni ya maisha na kuwa na hali bora ya maisha.

Mwisho wa maisha yangu ninapenda niwe nimefanya yafuatayo : Niwe nimepata nyumba bora ya kuishi ; nimpatie mzazi wa mahitaji yote ya muhimu ili naye apumzike maana amesumbuka sana kwa ajili yangu tangu kuzaliwa kwangu hadi sasa anaendelea kunihudumiwa ; niweze kuwa na vyombo vya usafiri ; nitoe huduma kwa wale wote wasiojiweza kama vile yatima, wajane, walemavu na wazee. Pia ninapenda kuwasaidia wote watakaohitaji msaada wangu.

Mwisho ninapenda niwe na familia ndogo itakayoishi kwa upendo, amani, umoja na ushirikiano katika mapenzi ya Mungu wetu.

Stella Iryarugo

DSC01637I am Stella Iryarugo, a 23-year-old Tanzanian. I am a girl who is creative, clever and inquisitive when it comes to education.

I am pursuing my education for the sake of my own future. Starting from elementary school until college, my goal has been to expand my understanding and to build a good life for myself.

The things I value in life include: my parents, who have worked hard to give me an education; Almighty God, who continues to grant me life; my dignity and the dignity of other people; and education. I value education because it is the source of knowledge and all other things. I value my studies, especially, my studies of art and science because they have helped me become more creative, clever and inquisitive.

I believe in the importance of my studies and all they have taught me, especially about teaching. Because I studied teaching at Katoke Teaching College, I will be an excellent teacher. I also believe in Mungu because of the life he has given me and that he grants you all that you ask him for.

My skills include playing various sports like netball, handball and gymnastics. I am also good at singing religious songs, and I have sung in several churches, including the Katoka Anglican Church. Another skill of mine is giving advice, especially advising my peers on good values and the importance of all people young and old.

My responsbility in life is to educate all people, especially young children and other students. Another responsibility I have is to raise my own children well, to educate them and to care for my family.

My short-term goal is to be an elementary school teacher. I just finished studying education, and I hope to be teaching at an elementary school in the near future.

At the end of my life, the things I would like to have achieved include: To have married and had four children, to have been a university professor and to have owned a good home and a car for my family.

Mimi Stella Iryarugo, raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 23. Mimi ni msichana ambaye ni mbunifu, jasiri na mdadisi katika mambo ya elimu.

Katika maisha yangu ninatafuta elimu kwa ajili ya maisha yangu ya baadae. Kuanzia elimu ya msingi mpaka chuo kikuu lengo ni kupanua taaluma yangu na kuweka mazingira mazuri ya baadae.

Mambo ninayothamini ni pamoja na wazazi wangu ambao wanakuwa kwa bega ili nipate elimu yangi, Mwenyezi mungu ambaye anazidi kunipa uhai, Utu wangu na wa watu wengi, na elimu. Nathamini elimu kwa kuwa ndio chanzo cha maarifa na chimbuko la mambo yote. Nathamini masomo yangu ninayosoma hasa masomo ya sayansi na sanaa kwa kuwa naongeza ubunifu, ujasiri na udadisi.

Ninaamini katika masomo yangu niliyoyapata kuwa nimeelimika hasa katika ngazi ya ualimu. Kutokana na mafunzo ya Ualimu niliyoyapata katika chuo cha ualimu Katoke nitakuwa mwalimu bora kuwafundisha wanafunzi. Pia ninaamini mungu kuwa kutokana na uhai pia na maombi mungu anakupa kila unachomuomba.

Vipaji vyangu ni pamoja na michezo mbalimbali kama netball, handball, pia michezo ya viungo, mfano kujitoma na kujifyatua. Pia nina kipaji cha uimbaji wa nyimbo za injiri nimeudumu katika kanisa mbalimbali ikiwemo Katoka Anglikane church. Kipaji changu kingine ni ushauri hasa kwa vijana wenzangu juu ya maadili na utii kwa watu wakubwa na wadogo.

Majukumu yangu katika maisha ni kutoa elimu kwa watu wote hasa watoto wadogo au wanfunzi, kuwafundisha na kuwapa elimu bora. Jukumu langu pia katika maisha yangu ni kuwalea watoto wangu katika msingi bora, pia kuwawezesha kupata elimu iliyo bora zaidi na kutunza familia yangu vizuri.

Malengo yangu ya muda mfupi ni kuwa mwalimu wa shule za msingi kutokana na mafunzo niliyohitimu hivyo nategemea kufundisha shule za msingi hapo baadae.

Malengo yangu ya muda mrefu ni kujiendeleza kutoka mwalimu wa shule za msingi hadi mwalimu wa chuo kikuu. Lengo likiwa ni kupanua maarifa yangu niliyonayo hili kukithi malengo yangu.

Mwisho wa maisha yangu mambo ninayotaka niwe nimeyakamilisha ni pamoja na : Niwe na familia yangu yaani niwe na mme wa ndoa, watoto wanne, niwe mwalimu wa chuo kikuu pia niwe ne nyumba nzuri na gari kwa ajili ya kutembelea mimi na familia yangu.

Nyangoso Machage

DSC01642

My name is Nyangoso Machage, and I am an 18-year-old Tanzanian.

I value many things in my life, such as my parents, the dignity of all people, my studies, my relatives and all other people in the world. I also value the different work, ideas and opinions of other people.

I believe that equality is the most important thing, and happiness is the number one thing I strive for in my own life.

My skills include being able to study biology and being a cheerful person. I am an excellent leader who works hard because I believe resting instead of working causes poverty for any person like me who is seeking a better life.

Right now in life I have one main responsibility that I cannot let anything distract me from, and that responsibility is to study hard day and night without listening to any people who might try to destroy my scholastic progress. After finishing my studies, my responsibility will be to help my community and the world at large by using my skills and education. Another responsiblity I have right now is to respect my parents, along with my friends and other relatives, because my parents are the pillars that have held me up for all of my successes.

My life goals can be broken down into two main categories, which are goals for the short term and goals for the long term.

My main long-term goal is to pass all of the tests in front of me, specifically I want to pass the Form 6 (12th Grade) test with Division I (highest marks) in Physics, Chemistry and Biology. I would then like to go study medicine at the University of West Virginia in America and to pass of all of my tests there as well. I also aim to marry a good wife who is cheerful, polite and full of love for her family and mine. I would like to live and work in New York City with my family. I will love my wife and my family more than I even love myself. Every now and then we will come to Tanzania to visit my parents and relatives.

My short-term goal is to study hard and to avoid all things that might pull me from the path of finishing my studies and achieving my dreams. I also have the goal of becoming a good listener who will be humble and listen to the advice of others.

I want a good life, which means for now I must concentrate only on my education and nothing else.

At the end of my life, I hope that I will have done the following things: I have studied and received my degree from West Virginian University; I have helped find vaccinations/cures for deadly illnesses like AIDS, cancer and malaria; I have married a good wife and had three children; I have lived in New York City with my wife and children; I have opened a hospital in Dar es Salaam, Tanzania.

In God I trust.

Mimi naitwa Nyangoso Machage. Nina umri wa miaka 18 na ni mtazania.

Katika maisha yangu nathamini mambo mengi kama vile wazazi wangu, utu wangu na wa watu wengine, masomo yangu na upendo wa hali ya juu sana kwa ndugu zangu wote pamoja na watu wengine. Pia ninaithamini kazi ya mtu mwingine na mawazo au maoni ya watu tofauti tofauti.

Katika maisha yangu ninaamini kuwa usawa ni jambo kuu na muhimu katika maisha na pia furaha ni jambo kuu lenye kufaa katika maisha yangu.

Vipaji nilivyonavyo ni kama ifuatavyo amabapo nina uwezo wa kusoma masomo ya sayansi ya viumbe na ni mchangamfu. Mimi ni kiongozi bora sana na pia ni mchapakazi mzuri ambapo ninaamini kuwa usingizi ni chanzo cha umaskini katika maisha ya mtu yeyote ule ambayo ni mtafutaji ama nilivyo mimi.

Majukumu niliyonayo katika maisha kwa sasa ninalo jukumu moja kuu ambapo sipaswi kulichanganya na jambo jingine lolote lile katika maisha yangu ya sasa na majukumu hilo ni kusoma kwa bidii usiku na mchana bila kujali ni mtu gani anayetaka kuniharibia mjongeo wangu au mwenendo wangu kimasomo. Pia jakumu langu nikiwa tayari nimemaliza masomo yangu ni kuisaidia jamii yangu na dunia kwa ujumula kwa kutumia ujuzi na elimu nitakatokuwa nimepata. Pia jukumu langu kingine la sasa ni kuwaheshima wazazi wangu na ndugu zangu na marafiki zangu. Maana wazazi wangu ndio nguzo na mwongozo katika kila mafanikio nimeyopata. Pia kuwapenda watu wote na kuufuata ushauri wao.

Malengo yangu katika maisha yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni malengo ya muda mrefu na malengo ya muda mfupi.

Malengo ya muda mrefu: Lengo langu kuu la muda mrefu ni kufaulu mitihani iliyopo mbele yangu yaani mtihani wa kidato cha VI ambapo ninefaulu kwa divisioni I PCB na endapo nitakuwa nimefaulu ningependa niende kusoma stashahada yangu ya udaktari katika chuo kikuu cha West Virginia kilichopo Marekani na kufaulu mtihani yote ya chuo hapo. Ambapo pia ninalenga kupata mke bora mwenye furaha, mchangamfu, mwenye nidhamu na mwenye kuwapenda na kuwajali ndugu zangu na ndugu zake ambapo makazi yangu kikazi itakuwa ni katika jiji la New York, Marekani, mimi na familia yangu. Nitampenda sana mke wangu na familia yangu kuliko nitakavyokuwa najipenda mimi mwenyewe. Mara kwa mara nitakuwa nikija Tanzania kuwaona ndugu zangu na wazazi wangu.

Malengo yangu ya muda mfupi ni kusoma kwa bidii zaidi na kuyaepuka yote ambayo yanaweza kunitoa katika mlolongo wa kuikamilisha ndoto yangu kuu hapo juu. Pia nina lengo la kuwa msikilizaji na mtu mwenye kujishusha na kusikiliza ushauri wa watu wengine.

Katika maisha yangu ninatafuta maisha mazuri yaani elimu kwa muda huu na siyo jambo jingine lolote lile ambalo linaweza kunitoa katika maendeleo ya elimu yangu kwa ujumla.

Mwisho kabisa wa maisha yangu ningependa kuwa nimeyafanya yafuatayo: Nimepata elimu yangu ya chuo kikuu katika West Virginia Univerity; Nimetafuta chanjo ya magonjwa hatari kama UKIMWI, kansa na malaria; Nimempata mke mzuri na watoto watatu; Nimefanikiwa kuweza kuishi jijini New York mimi na familia yangu; Nimefungua hospitali jijini Dar es Salaam

In God I Trust.

Raulian Raphael

DSC01643

My name is Raulian Raphael, a male Tanzanian. During my lifetime, the thing I most important thing is that I work for and achieve all of my dreams, especially my goal of helping create jobs for young people.

There are several things I value, including human rights, equality and education. These things will bring all of us people together so that we can work to develop our world without harassment, discrimination and opprestion.

As a whole, I believe there two important things in life: to commit oneself and work hard. These two are the two pillars necessary for encouraging development and combating poverty. When people are healthy and whole, everything is possible and all people are equal.

Furthermore, I have skills that will help me to achieve my goals, such as drawing and playing sports like the high jump and running. These skills make me a cheerful, healthy person, and they help me to be creative in things concerning the arts and sciences.

However, I have more than just skills and dreams, I also have certain responsibilities in my life. One of these is to study hard, to educate my community and to defend human rights and equality in my community. Doing this will ensure peace and security, which are the cornerstones of development throughout the entire world.

My short-term goals are to study, to help protect our environment by planting trees and to protect my rights and the rights of my community. My main goals for later in life are to become a doctor so that I can work to find a cure for chronic, dangerous illnesses like cancer and strokes that cause many deaths all across the world.

At the end of my life, I want to have accomplished several important goals. The first is to build a big hospital and a center that will help orphans, the elderly, children in need and people with disabilities. I also want to perform scientific research and help ensure that rights and equality of all people. Simultaneously, I also hope to help find a way to address the lack of jobs available for young people.

Kwa majina ninaitwa Raulian Raphael. Ni kijana wa kiume raia wa Tanzania. Katika maisha yangu jambo kuu ninalolitafuta ni kuzifikia na kukamilisha ndoto zangu hasa upatikanaji wa ajira kwa vijana.

Katika maisha yangu mambo ninayothamini ni pamoja na haki, usawa pamoja na elimu bora. Mambo hayo kwa pamoja yataweza kutuweka binadamu wote pamoja hivyo kuweza kujiletea maendelea sisi wenyewe bila unyanyasaji, ubaguzi na hata ukandamizaji.

Kwa ujumla maishani mwangu naamini sana kuu ya mambo makuu mawili ambayo ni kujituma na kufanya kazi kwa bidii kuwa ndio misingi mikuu ya kuleta maendelea pamoja na kupambana na umaskini. Hivyo palipo afya na uzima kila kitu chawezekana, na binadamu wote ni sawa.

Hali kadhalika, ninavyo vipaji vitakavyoweza kunisiadia kuyafikia malengo yangu na vipaji hivi ni uchoraji, michezo kama vile miruko ya juu na kukimbia. Vipaji hivi hunifanya kuwa mchangamfu na mwenye afya na kuniongezea ufanisi katika ubunifi wa kisayansi na kisanaa.

Si mambo haya tu lakini pia ninayo majukumu makubwa sana katika maisha yangi. Moja ya majukumu haya ni kusoma kwa bidii, kuelimisha jamii, kutetea haki na usawa katika jamii hii ni ajili ya kuhakikisha amani na usalama kuwa ndio misingi ya maendelea duniani kote.

Malengo yangu ya mda ni kusoma na kujihusisha na utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti ya kutosha, kudai haki zangu stahili pamoja na haki za jamii yangu. Mbali na hayo malengo yangu makuu ya hapo baadaye ni kuwa daktari na hii ni kwa ajili ya kupata suluhu la magonjwa sugu na hatari sana kama vile kansa pamoja na kupooza, kwani yamekuwa chanzo cha vifo vingi sana duniani sehemu mbalimbali ulimenguni.

Mwisho wa maisha yangu ninapenda kuwa nemekamilisha mambo haya muhimu, kujenga hospitali kubwa na kituo cha kulelea watoto yatima, pamjoa na kusaidia wazee, watoto pamoja na walemavu. Ikiwa ni pamoja na kuendesha utafiti na uchunguzi wa kisayansi, pia kuhakikisha haki na usawa umepatikana kwa watu wote sanjari na kutatua na kulipatia ufumbuzi suala la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Alistidia Florian

I am Alistidia Florian, a Tanzanian girl who is 19 years old. I finished Form IV (10th grade) in 2013 at Kayanga Secondary School. I am confident, respectful and care for all people, whether they be old or young, rich or poor.

I seek human rights, education and equality for all people. I value human dignity, agriculture, my parents, education and God. All people have the right to dignity and to be respected, even if they are young, disabled or any other type of person. Education is especially important because it delivers us from hardship. Without education, you will not be as valued by other people. I also really value my parents because they are second only to God. I love them, and they have provided me with the education that has continued to help me even up until this point in my life.

I believe that all things are possible if you pray to God. If you don’t just depend on yourself and instead you believe in and ask God for help, your goals will be achieved. Whether you want to be a doctor, teacher or lawyer, if you ask you will receive because God himself has said that as you believe, so it shall be.

I also believe education makes all things possible because if you are educated you will have a purpose in life. If you are education, it is easier to find good work, and because of this education is my main focus in life now.

I also believe money helps makes all things possible. Money helps people to gain their rights. Many people have lost their rights because of money, so this is why I believe money is important.

My skills are playing soccer, playing mchezo wa pete, and teaching. After finishing Form IV, I volunteered to teach small children, and I am very good at teaching art.

My responsibilities in life are to study hard in order to help me achieve my goals and to help with chores and home. My short-term goal is to continue with my studies, and my long-term goal for after I finish studying is to help my family, to help those in need and to become the leading lawyer in Tanzania who will help people protect their rights regardless of race, tribe or political affiliation.

The first thing I want to have accomplished at the end of my life is to have helped those in need like orphans, widows and people with disabilities to gain an education and other important life necessities. I also want to have help those who have been oppressed by laws, such as widows who have their wealth and inheritance snatched away. As a lawyer, I also want to have helped combat corruption and punish both those who give and receive bribes of any kind.

Mimi ni Alistidia Florian ni msichana wa kitanzania mwenye umri wa miaka 19. Ni mhitimu kidato cha nne mwaka 2013 katika shule ya sekondari Kayanga. Mimi ni kijana mwenye ujasiri, heshima, na utii kwa kila mtu mdogo kwa mkubwa na tajiri kwa maskini.

Mimi katika maisha yangu natafuta haki, elimu, pamoja na usawa kwa kila mtu. Katika maisha yangu nathamini utu wa mtu, kilimo, wazazi, elimu pamoja na Mungu. Kila mtu ana haki ya kutunzwa utu wake na heshima yake awe mdogo, mlemavu, au mtu yeyote yule. Pia nathamini sana elimu kwa sababu ndio mkombozi wetu. Pasipo elimu huwezi kuwa na thamani mbele ya watu. Pia wazazi wangu nawathamini sana kwa sababu ndio Mungu wa pili ukitoa tule wa mbingu. Nawapenda na ndio wanaonipa elimu ambayo inanisiadia mpaka sasa kwa hiyo nawapenda sana.

Mimi ninaamini katika Mungu kwamba kila akitu kinawezekana ukimuomba Mungu. Hukujiwekea malengo na ukamuomba Mungu na kumuamini lazima lengo lako litatimia. Ukiwa na lengo la kuwa daktari, mwalimu, au mwanasheria na ukimwomba lazima utapata kwa sababu yeye alisema unavyoamini ndivyo itakwavyokuwa.

Pia naamini katika elimu kwa kila kitu kinawezekana na ukiwa na elimu yako, huwezi kuangaika. Ukiwa elimu itakuwa rahisi kupata kazi nzuri na ya maana kwa hiyo elimu kwangu ndio mpango mzima.

Pia naamini katika pesa kwamba kila kitu kinawezekana ukiwa na pesa. Pesa inaweza kununua hata roho ya mtu. Pesa inafanya mwenye haki asiwi na haki. Wengi wamepoteza haki zao kwa sababu ya pesa kwa hiyo naamini katika pesa kila kitu kinawezekana.

Vipaji vyangu ni kucheza mpira wa miguu, kucheza mpira wa pete na kufundisha. Baada ya kuhitimu kidato cha nne, nilikuwa najitolea kufundisha watoto wadogo na pia nina uwezo katika kufundisha mambo ya sanaa.

Majukumu yangu katika maisha yangu ni kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yangu, pia kusaidia kazi ndogondogo za nyumbani. Malengo ya muda mfupi ni kusoma na malengo ya muda mrefu baada ya masomo ni kusaidia familia yangu, kuwasaidia wahitaji, pia kuwa mwanasheria mkuu wa Tanzania na kutoa haki kwa wote bila kuchagua rangi, kabila au chama.

Mambo ambayo nataka niwe nimeyakamilisha niwe nimeshawasaidia wahitaji hasa yatima, wajane na walemavu kwa kuwapatia elimu na mahitaji muhimu katika maisha. Pia kuwa nimewasaidia wale wanakandamizwa na sheria kama wanawake wajane wanaonyanganywa mali zao. Pia kama mwanasheria ni kupigana na rushwa kwa wale wanaotoa au kupokea rushwa ya aina yoyote ile.

Advertisements

4 Responses to Our Teachers

  1. Fahim Ally says:

    Nimefurahi sana kuona kitu kama hiki! kwakweli UONGOZI WA THE OTA INITIATIVE MMEFANYA KAZI NZURI SANA! Asanteni sana!

  2. mmenifurahisha kuleta mabadiliko ya elimu hapa Karagwe mimi nitazidi kuwa mdau wenu
    you have made me happy for making changes of Education in Karagwe i will continuing to work with you.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s